Ya Bungeni ni matunda ya soko la kura...

Ya Bungeni ni matunda ya soko la kura...
29 June 2011


Ni hatari, si salama na wala sio busara kuacha hatima ya taifa letu iamuliwe kwa mujibu wa maslahi ya soko la kura. Soko ambalo kwa muda mrefu tumekuwa tunalidumaza kifikira. Soko ambalo badala ya kuwa mkombozi wa mtanzania limegeuzwa kuwa janga la utaifa wetu. Soko lililogeuzwa kuwa mazalia  uozo wa kisiasa. Soko ambalo kamwe halitaweza kutuondoa katika lindi la maadui umasikini, ujinga, maradhi, ufisadi na ubaguzi.

Bunge letu la sasa ni matunda ya mfumo na utamaduni wa kisiasa unaojengek​a wenye kuweka mbele maslahi ya soko la kura na kusahau ama kudharau wajibu wa uongozi na kamwe sio kupanuka kwa demokrasia.

Wakati wanasiasa wetu wanaamini kuwa siasa za kukosa busara na staha dhidi ya "Watawala" zinashabikiwa na vijana wengi hivyo ni mtaji muafaka wa kura, wamesahau uongozi ni dhamana na una majukumu yake!

Kimsingi baadhi yao wanaamini kuwa hizo ndio siasa zinazovutia wapiga kura vijana. Hawajali wajibu wao kama viongozi. Wanasahau ni Tanzania wanayoijenga sasa ndiyo wayakayopaswa kuitawala wakishika dola.

Lakini zaidi ufinyu wa ustadi katika siasa za kujenga zenye kuambatana na uerevu wa masuala ya kitaifa na kidunia katika uga wa siasa unapelekea baadhi ya wanasiasa wetu kuamini katika siasa za ujanjaujanja ili kuficha mapungufu yao. 

Naweza kusema hili ni zao historia ndefu ya nchi yetu kujikita katika utoaji wa bora elimu na pia tatizo la ukosefu wa watu wenye ujuzi, uwezo na umahiri wa masuala mbalimbali ya kimaendeleo katika platform za siasa kama bunge letu.

Lakini pia ukosefu wa hulka ya uthubutu miongoni mwa watanzania wenye elimu bora, misingi thabiti na umahiri wa masuala ya uongozi na siasa kuingia katika taaluma ya siasa na kukimbilia maeneo salama kimaisha na kimaslahi.

Kwa upande mwengine soko hili la kura limefanikiwa kutupa viongozi tunaowaona na wakaendelea kupata  ushabiki na hata ufuasi miongoni mwetu hasa sisi vijana kutokana na miaka mingi ya matumizi mabaya ya imani ya watanzania. Imani ambayo watanzania waliwapa viongozi wao pamoja na asasi za utawala. 

Ni kutokana na tabia za baadhi ya viongozi wetu kutumia vibaya imani na ridhaa ya watanzania hata kufikia kuwadhihaki na kuwabeza huku wakishindwa kutatatua hata ya matatizo ya msingi ya wananchi hao nako kumewezesha wanasiasa wajanjawajanja kuchakachua soko la kura. 

Uchakachuaji ambao badala ya kuwapa nafasi watanzania kuwa na upeo mkubwa wa kuchagua viongozi bora unawafanya wawe wahanga wa kuchagua viongozi wahuni zaidi, walafi zaidi, wazembe zaidi na wabinafsi zaidi.

Ili kuepukana na hatari hii ni wajibu wetu sote kuwa mstari wa mbele kujenga upya misingi ya siasa safi na uongozi bora. Na hili litafanikiwa endapo sote ambao tumebarikiwa kupata elimu na kujengeka kifikira kukataa kuwa wahanga wa siasa zenye kujali na kuamini katika kasumba za kisiasa badala Ukweli wa mambo. 

Lakini pia kuwa tayari kuhakikisha kuwa kila mtanzania anapaswa kujua ukweli wa mambo na kumuepusha kuwa mhanga wa siasa za kasumba, hovyohovyo na majitaka. Siasa ambazo huwezesha udumavu wa kifikira na pia kuwa mtaji wa wanasiasa wajanjawajanja, wahuni na hata madhalimu wanaojivika vilemba vya uwanamapinduzi, uzalendo na ukombozi. Wanasiasa ambao wako tayari kuweka rehani mustakbali wa taifa letu kwa maslahi yao ya kisiasa na binafsi.

Nelson Mandela Leadership Philosophy and my Zanzibarinjema Dream.

 Happy Birthday Mzee Madiba.

Though I abhor the western pimping-iconization of #NelsonMandela, I duly admire and salute his unshaken philosophy of forgiveness n rainbow nation.  

To understand the value of Nelson Mandela philosophy Tanzanians need to look Zanzibar timulutous history.   

Zanzibar timulutous history of never ending sociopolitical cleavages has dwarf all it's economic power potential.  

While we now have a new Gov of National Unity dispensation in #Zanzibar, more needs done to protect and nurture the  spirit of cooperation in making Zanzibarinjema.  

The noble leadership of three genuine and humble brothers, Ally Shein, Seif Sharif and Ali Seif Idi, needs be supported by institutions of forgiveness, trust and hope above all.  

For this to be achieved and sustain above the three personalities and the constitution, a culture of constructive engagement and embracing of the power of diversity is paramount.  

More, I sometime think maybe we should dare to establish Kamisheni ya Ukweli, Uwazi na Maelewano!

Mtazamo wangu kuhusu majibu ya Zitto dhidi ya makala ya leo katika gazeti la Tanzania Daima

Mtazamo wangu kuhusu majibu ya Zitto dhidi ya makala ya leo katika gazeti la Tanzania Daima.


Sifa kuu za mbumbumbu wa siasa ni kupenda na kuamini katika siasa chafu, wivu na uadui! Ni wazi kinachofanywa na wahariri wa gazeti hilo linalomilikiwa na mwenyekiti wa chama chake ni mfano halisi wa umbumbumbu wa siasa.

Shutuma dhidi ya Zitto kwa kulalamika mtandaoni kuhusiana na kitendo hicho cha Tanzania Daima kuandika habari yenye nia mbaya kwake zinaonyesha kuwa kuna watu wangependa kuona Zitto anakufa kisabuni. Mpaka Zitto alipofikia kureact namna hii ni wazi kuna juhudi alizofanya kuleta busara miongoni mwa viongozi wenzake ambao ukweli ni kuwa wengi wao wanaamini ili wafanikiwe wao ni lazima Zitto aangamizwe bila ya kujali kuwa in a way wanaangamiza chama chao. 

Lakini pia hii tabia ya kutumia busara ya kuepusha taswira ya mgawanyiko ama mgogoro ndani ya Chadema katika kufunika uozo wa ubadhirifu aka ufisadi na siasa chafu zenye kujaa chuki haina tofauti na ile ya wenzao wa CCM ya kutumia Amani na Utulivu katika kufunika uozo wao. Ni wazi athari ya kuamini katika ujanjaujanja huo zinainekana zinavyowazamisha kama chama na taifa kwa ujumla.

Maadui wa kweli wa umoja, amani na utulivu ama ndani ya vyama vyenu ama nchi yetu ni wale wanaonajisi umoja, amani na utulivu huo kwa kuendeleza ubadhirifu aka ufisadi, siasa chafu, wivu na chuki na sio wale wanaothubutu kusimama kuonyesha, kukemea na kujitetea dhidi ya uharamia huu wa kisiasa na hata kimaisha

Lakini pia yawezekana kwa kuwa wengi hawajui ni mangapi amenyamazia ndio maana baadhi wanasisitiza busara ya kunyamaza. Wakati wanaona kuwa ni busara kwa Zitto kunyamaza wenzake  wanachukulia kama udhaifu na mtaji katika kufanikisha nia yao mbaya iliyojikita katika utamaduni wa kuamini katika siasa chafu. 

Wakati wengi wanasisitiza Zitto kunyamaza kwa maslahi ya chama chao wenzake busara hiyo hawana na kwa muda mrefu sasa wamekataa kuitambua. Busara ya kunyamaza huku wenzako wakikumaliza inageuka ujinga pale inapohusu wasio amini katika busara hiyo.

Kwa ujumla ni vizuri maadui wake wanajianika ili watu watambue nia zao chafu na mipango yao haramu!