17 July 2012
Hatimaye Amir Mkuu wa Kweli wa UAMSHO Ndugu yangu Ismail Jussa afunguka baada ya kuona kuwa vijana wake wameweza kufanya kazi ya kutosha kuipa sura ya UZANZIBARI na sio CUF pekee agenda ya JAMHURI YA ZANZIBAR YENYE MAMLAKA KAMILI NDANI NA NJE NA KUWA NA KITI CHAKE UN ( meaning kuvunja muungano) na baadaye KUFANYA MUUNGANO WA MKATABA (meaning Ushirikiano hafifu kuliko ule wa EAC).
Uthubutu huu wa Jussa kuonyesha wazi uongozi wake katika vuguvugu la UAMSHO ambalo limekuwa likilenga MUUNGANO, UKRISTO Na WATANGANYIKA kama maadui wa USTAARABU na Maendeleo ya Zanzibar umekuja baada ya vijana wake wa CUF waliokuwa wakizunguka kila mahala ambapo Tume Ya Katiba Mpya ilipokuwa ikienda katika Mkoa wa Kusini Unguja ambao unafahamika kama ngome ya CCM kumtaarifu kuwa kati ya watoa maoni, Asilimia 48 waliongelea ajenda ya CUF-UAMSHO ya kuwa na Jamhuri ya Zanzibar yenye Mamlaka Kamili (full sovereignty) ndani na nje na kuwa na kiti chake katika UN, Rais wake anayetambulika ndani na nje ya Zanzibar, Fedha yake, Elimu yake, na Mafuta na Gesi yao pekee huku wengine asilimia 48 kutaka kuendelea na mfumo wa muungano wa sasa lakini kushughulikia matatizo ya Muungano.
Yaani hii ndio athari ya spinning... Unaandaa vijana wako kuwa vocal ktk kila pande ya nchi halafu unajiaminisha kuwa weee una wengi kuliko wenzako. Jussa anajua kuwa ktk kila mkutano wa maoni kulikuwa na kiongozi wa CUF aliyekuwa akicoordinate utoaji wa maoni kwa vijana waliokuwa recruited maalum kwa kushindana na maoni ya wenyeji wengi wa maeneo hayo. Hata maoni hayo yalionekana wazi kufanana kama kujirudiarudia kuanzia nukta hadi nukta na hata watoaji maoni kuwa na karatasi moja iliyochapishwa kwa computer. Na zaidi taarifa nyingi alizokuwa akipewa ndugu yangu Jussa zilikuwa zimechakachuliwa kuonyesha hali nzuri kwa uwasilishaji wa maoni yanayoendana na ajenda ya CUF- UAMSHO.
Ndugu yangu Jussa, moja ya kitu muhimu ni kutambua na kukubali ukweli kuwa Zanzibar imegawanyika. Mgawanyo wa madaraka kwa wakubwa tu hautoshi kuondoa mgawanyiko wa Wazanzibari. Umoja unaotaka tu uone utaweza kujengwa kwa kwanza kuwa na MCHAKATO WA TUME AMA KAMATI YA UKWELI, UWAZI NA MARIDHIANO ya wazanzibari wote na still itachukua generations kuondoa huwa mgawanyiko na kujenga umoja wa kihalisia. Kushikamana dhidi ya adui Tanganyika cum Ukristo haitoshi kujiaminisha kuwa ni wamoja.
Maoni anayoripoti Jussa kwa ajili ya kujenga ama kuhalalisha ajenda ya CUF kuwa ni ya Wazanzibari wote ama wengi ambayo ingawa kuna mengi amekosea/kupotosha ama anapotoshwa na mengine hajaripoti yanaweza kuangaliwa kama mafanikio ya vuguvugu la UAMSHO.
Ni wazi kuwa matumizi na strategy ya UAMSHO ina uungwaji mkono wa wasiokubaliana na ajenda kuu ya UDINI ya UAMSHO, yaani wale kutoka HIZBU cum CUF na CCM cum ASP masalia wamekuwa wadau wa harakati za UAMSHO. Wakati ni wazi kuwa UAMSHO ni tawi la siasa za CUF wasizoweza kuzifanya katika mazingira ya SERIKALI YA PAMOJA, Ni wazi pia vuguvugu la UAMSHO lina wadau wa pande zote za kisasa na kijamii katika Zanziba.
Wote kwa upande wa HIZBU-CUF na CCM- ASP masalia wanaamini katika kutumia UAMSHO kujenga mazingira ya majadiliano yatakayoweza kulazimu wauumini wa MUUNGANO thabiti katika mchakato huu wa katiba mpya kuwa tayari kucompromise kwa kutoa madaraka zaidi ya ZANZIBAR hasa yale yaendanayo na UTAMBULISHO wa UZANZIBARI (Zanzibar Pro Arab cum Islam Identity - nationalism) kwanza kwa upande mmoja na UHURU wa kumalizana wenyewe kwa upande mwengine (CCM - ASP masalia wanaoamini kuwa MUUNGANO unawazuia kuendeleza dhana ya Mapinduzi Daima).
Wote wanakubaliana katika kutukuza UZANZIBARI KWANZA ingawa naamini hawajatambua athari ama challenges za mashirikiano haya ya sasa huko tuendako. Ofcourse kuna wengine wana maslahi yao hasa unyang'anyi waliokuwa wakiufanya dhidi ya wazanzibari na ili kulinda maslahi yao dhidi ya uwezekano wa Uongozi wa Serikali ya Pamoja kuchukua hatua za kurekebisha ufisadi uliokuwa ukiendelea katika tawala za nyuma sasa wameamua kuungana na CUF-UAMSHO ili kumtikisa Rais Shein na Makamu wa Rais wake wasipate nafasi ya kuyanhughulikia mambo hayo. Ni wazi ndugu zangu wameshindwa kusoma alama za nyakati kutoka kwa yanayotokea MALI kwa muktadha ANSAR DEEN na TUAREGS ambayo ni somo muhimu kutiliwa maanani katika haraka zao.
Kimoja anachosahau ama kutojali ndugu yangu Jussa ni kuwa Tanganyika ama watanganyika hawaihitaji sana Zanzibar hadi kuwa tayari na UNDUGU wa kutokuaminiana na uliojaa chuki dhidi yao. Zaidi kwa mwenendo huu Wazanzibari wasishangae watanzania watakapokuja kuwa maadui wa Zanzibar na Maswahiba wa Kenya katika safari ya Ujenzi wa Shirikisho au Muungano wa AFRIKA MASHARIKI. Sasa tutegemee motion ya Kuvunja Muungano katika Baraza la Wawakilishi hivi karibuni...