Mtazamo wangu kuhusu majibu ya Zitto dhidi ya makala ya leo katika gazeti la Tanzania Daima

Mtazamo wangu kuhusu majibu ya Zitto dhidi ya makala ya leo katika gazeti la Tanzania Daima.


Sifa kuu za mbumbumbu wa siasa ni kupenda na kuamini katika siasa chafu, wivu na uadui! Ni wazi kinachofanywa na wahariri wa gazeti hilo linalomilikiwa na mwenyekiti wa chama chake ni mfano halisi wa umbumbumbu wa siasa.

Shutuma dhidi ya Zitto kwa kulalamika mtandaoni kuhusiana na kitendo hicho cha Tanzania Daima kuandika habari yenye nia mbaya kwake zinaonyesha kuwa kuna watu wangependa kuona Zitto anakufa kisabuni. Mpaka Zitto alipofikia kureact namna hii ni wazi kuna juhudi alizofanya kuleta busara miongoni mwa viongozi wenzake ambao ukweli ni kuwa wengi wao wanaamini ili wafanikiwe wao ni lazima Zitto aangamizwe bila ya kujali kuwa in a way wanaangamiza chama chao. 

Lakini pia hii tabia ya kutumia busara ya kuepusha taswira ya mgawanyiko ama mgogoro ndani ya Chadema katika kufunika uozo wa ubadhirifu aka ufisadi na siasa chafu zenye kujaa chuki haina tofauti na ile ya wenzao wa CCM ya kutumia Amani na Utulivu katika kufunika uozo wao. Ni wazi athari ya kuamini katika ujanjaujanja huo zinainekana zinavyowazamisha kama chama na taifa kwa ujumla.

Maadui wa kweli wa umoja, amani na utulivu ama ndani ya vyama vyenu ama nchi yetu ni wale wanaonajisi umoja, amani na utulivu huo kwa kuendeleza ubadhirifu aka ufisadi, siasa chafu, wivu na chuki na sio wale wanaothubutu kusimama kuonyesha, kukemea na kujitetea dhidi ya uharamia huu wa kisiasa na hata kimaisha

Lakini pia yawezekana kwa kuwa wengi hawajui ni mangapi amenyamazia ndio maana baadhi wanasisitiza busara ya kunyamaza. Wakati wanaona kuwa ni busara kwa Zitto kunyamaza wenzake  wanachukulia kama udhaifu na mtaji katika kufanikisha nia yao mbaya iliyojikita katika utamaduni wa kuamini katika siasa chafu. 

Wakati wengi wanasisitiza Zitto kunyamaza kwa maslahi ya chama chao wenzake busara hiyo hawana na kwa muda mrefu sasa wamekataa kuitambua. Busara ya kunyamaza huku wenzako wakikumaliza inageuka ujinga pale inapohusu wasio amini katika busara hiyo.

Kwa ujumla ni vizuri maadui wake wanajianika ili watu watambue nia zao chafu na mipango yao haramu!

No comments: