Salaam kutoka Ardhi ya Wapalestina


Salaam kutoka Ardhi ya Wapalestina: Jana jioni nimewasili katika mji wa Ramallah baada ya kukaa katika mpaka wa Palestina na Jordan unaosimamiwa na Waisrael kwa muda wa masaa matatu. Tofauti na picha niliyokuwa nayo hapo kabla kuhusu mji huu ulio chini ya ukoloni wa Waisraeli na uliowahi kukumbwa mashambulizi kadhaa ya majeshi ya Waisrael likiwemo lile lilomuweka kizuizini Comrade Arafat kwa miaka kadhaa kabla ya kuawa na sumu, mji huu ni mji mzuri kupita kiasi. Ni mji mzuri mara kadhaa zaidi ya miji yetu mingi ya kiafrika kama Dar es Salaam. Nategemea kuwa huku kwa wiki nzima kama mgeni wa Wapalestina nikiwa na wenzangu wanne kutika Tanzania na marafiki wengine wa Wapalestina kutoka nchi kadhaa duniani. Kitu kimoja nilichokutana nacho jana mara nilipofika hotelini ni kukutana na mzee mmoja katika lifti ambaye baada ya kujua natoka tanzania akaniambia "Karibu sana Palestina" kwa kiswahili fasaha. Then akanieleza kuwa ametembelea sehemu mbalimbali za Tanzania kwa mara kadhaa na ni rafiki mkubwa wa Mwalimu, Mkapa na Salim Ahmed Salim. Baadae akanichukua kwa meneja wa Hoteli na kumuambia kuwa mimi ni rafiki yake... "Ndugu yangu huyu. Take good care of him" Baada ya kumuuliza sana ananiambia alikuwa mshauri wa Arafat kwa miaka mingi na kunipa kadi yake ili niwasiliane naye kwa chochote kile nitakachotaka. Tukio hili limeniongezea majivuno yangu ya kuwa MTANZANIA! Proudly Tanzaniana forever! 

Leo ni shughuli maalum ya kumbukumbu ya mauaji ya Comrade Arafat na kutembela kaburi lake! Safari yangu nategemea kunifikisha Bathlehem, Nazareth, Jerusalem, Neblus, Jericho na sehemu nyingine mbalimbali ikiwemo kambi za wakimbizi wa kipalestina waliondolewa katika maeneo yao na utawala wa kimabavu wa Waisraeli na pia ukuta wa ubaguzi!

No comments: